Surat An-Nisa, aya 16

4:16

وَٱلَّذَانِ يَأۡتِيَٰنِهَا مِنكُمۡ فَـَٔاذُوهُمَاۖ فَإِن تَابَا وَأَصۡلَحَا فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابٗا رَّحِيمًا ١٦

Walladhāni ya'tiyānihā minkum fa'ādhūhumā fa in tābā wa aslahā fa a'ridū 'anhumā innallāha kāna tawwābar rahīmā

Na wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu. 16

Maelezo ya chini

16 Mwanamume na mwanamke walio zini, nao hawajaoa (au kuolewa), wapewe adhabu maalumu, pindi ikithibiti hiyo zina kwa mashahidi wane waadilifu. Wakitubu baada ya kupewa adhabu, basi msiwatajie hayo maasi waliyo yatenda, wala msiwaaziri. Hakika Mwenyezi Mungu kwa rehema yake anakubali toba ya wenye kutubu.