Surat An-Nisa, aya 139

4:139

ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا ١٣٩

Alladhīna yattakhidhūnal-kāfirīna awliyā'a min dūnil-mu'minīna ayabtaghūna 'indahumul-'izzata fa innal-'izzata lillāhi jamī'ā

Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. 139

Maelezo ya chini

139 Hao wanaafiki huufanya utawala wa makafiri uwe juu yao, na wanawawacha Waumini. Basi hebu hivyo wanataka wapate utukufu kwa hawa makafiri? Hakika utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye huwapa waja wake wenye kuamini. Na mwenye kutaka utukufu kwa Mwenyezi Mungu atatukuka, na mwenye kutaka utukufu kwa mwenginewe atadhalilika.