وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغۡنِ ٱللَّهُ كُلّٗا مِّن سَعَتِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمٗا ١٣٠
Wa in yatafarraqā yughnillāhu kullam min sa'atihī wakānallāhu wāsi'an hakīmā
Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima. 130
Maelezo ya chini
130 Ikiwa suluhu haikumkinika na ikawa chuki (au karaha) imeshika nguvu zaidi, basi inalazimika kufarikiana. Na wakifarikiana Mwenyezi Mungu atawatosheleza kila mmoja wao kutokana na ukunjufu wa rehema yake na fadhila yake. Na riziki ziko katika mikono ya Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye hikima, na hupanga mambo yote kwa mipango yake.