فَلَا تَضۡرِبُواْ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡثَالَۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ٧٤
Falā tadribū lillāhil-amthāla innallāha ya'lamu wa antum lā ta'lamūn
Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua,na nyinyi hamjui. 74
Maelezo ya chini
74 Na ilivyo kuthibitikieni kuwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu hakufaeni kitu, basi msiseme kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ana yeyote wa kumshabihi, ikawa kisingizio cha kuwaabudu hao kwa vipimo vipotovu, na kushabihisha kusio kweli kwa ajili ya kuwaabudu hao pamoja naye! Hakika Mwenyezi Mungu anajua upotovu wa mnayo yatenda, naye atakulipeni kwayo na hali nyinyi mmo katika mghafala hamjui ubaya wa mwisho wenu!