وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ ٤٩
Walillāhi yasjudu mā fis-samāwāti wamā fil-ardi min dābbatin wal-malā'ikatu wahum lā yastakbirūn
Na vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi, tangu wanyama mpaka Malaika, vinamsujuidia Mwenyezi Mungu, na wala havitakabari. 49
Maelezo ya chini
49 Ni kwa Mwenyezi Mungu pekee - wala si kwa mwenginewe - hunyenyekea na kut'ii vyote alivyo viumba mbinguni na viumbe viliomo na vyendavyo katika ardhi. Na mbele yao ni Malaika wanao nyenyekea wala hawatakabari na kumt'ii. Aya hii imeitangulia sayansi kwa kusema kuwa katika baadhi ya sayari upo uhai katika mfumo huu wetu wa jua, au nje yake. Sayansi sasa inajaribu kutaka kuvumbua hayo.