Surat An-Nahl, aya 41

16:41

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ٤١

Walladhīna hājarū fillāhi mim ba'di mā zulimū lanubawwi'annahum fid-dunyā hasanatan wala'ajrul-ākhirati akbaru law kānū ya'lamūn

Na wale walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa,bila ya shaka tutawaweka duniani kwa wema; na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti kuwa wanajua! 41

Maelezo ya chini

41 Na Waumini walio yaacha majumba yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na usafi wa imani yao, baada ya kudhulumiwa na washirikina, tutawalipa duniani, kwa ikhlasi yao na kustahamili kwao adhabu, maisha mema yasiyo patikana ila kwa jihadi. Na Siku ya Kiyama ujira wao utakuwa mkubwa zaidi, na neema zao za Peponi ni kubwa zaidi. Lau kuwa wapinzani wao wangeli jua hayo wasingeli wadhulumu na wakazidhulumu nafsi zao.