إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ ٤٠
Innamā qawlunā lishay'in idhā aradnāhu an naqūla lahū kun fayakūn
Kauli yetu kwa kitu tunacho kitaka kiwe, ni kukiambia: Kuwa!Basi kinakuwa. 40
Maelezo ya chini
40 Na kuwafufua watu Siku ya Kiyama si jambo zito kwetu, hata hao makafiri wakayaona hayawi. Kwani Sisi tutakapo kitu kiwe hatuna haja ya lolote ila ni kusema tu: Kuwa! Na kinakuwa kama tutakavyo.