لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ ٣٩
Liyubayyina lahumul-ladhī yakhtalifūna fīhi waliya'lamal-ladhīna kafarū annahum kānū kādhibīn
Ili kuwabainishia yale waliyo khitalifiana, na ili wajue waliokufuru kwamba wao walikuwa ni waongo. 39
Maelezo ya chini
39 Hakika katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kuwa atawafufua wote baada ya kufa kwao ili ipate wadhihirikia hakika ya mambo waliyo khitalifiana. Waumini wapate kujua kuwa wao wako katika Haki, na makafiri wajue kwamba wao walikuwa makosani kwa kumfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika Ungu, na pia ni waongo kwa kuapa kwao kwamba Mwenyezi Mungu hamfufui aliye kufa, na ili yote makundi mawili yapate malipo yao kwa kujua na kwa sababu zake.