Surat An-Nahl, aya 23

16:23

لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ ٢٣

Lā jarama annallāha ya'lamu mā yusirrūna wamā yu'linūna innahū lā yuhibbul-mustakbirīn

Hapana shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza. Kwa hakika Yeye hawapendi wanao jivuna. 23

Maelezo ya chini

23 Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza, ikiwa ni itikadi au maneno au vitendo. Naye atawahisabu kwa yote hayo, na atawaadhibu kwa kiburi chao. Kwani hakika Yeye Subhanahu hawapendi wanao jivuna hata hawataki kusikia Haki na kuifuata.