Surat An-Nahl, aya 19

16:19

وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ ١٩

Wallāhu ya'lamu mā tusirrūna wamā tu'linūn

Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. 19

Maelezo ya chini

19 Na Mwenyezi Mungu kwa ujuzi wake ulio kusanya kila kitu, anajua mnayo yaficha na mnayo yadhihirisha. Na hapana chochote kinacho fichikana kwake cha siri yenu na jahari yenu.