Surat An-Nahl, aya 18

16:18

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ ١٨

Wa in ta'uddū ni'matallāhi lā tuhsūhā innallāha laghafūrur rahīm

Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu. 18

Maelezo ya chini

18 Na mkitaka kuzihisabu neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu wa rehema. Basi tubuni kwake, na mumsafie ibada, ili apate kukusameheni na kukurehemuni.