Surat An-Nahl, aya 127

16:127

وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ ١٢٧

Wasbir wamā sabruka illā billāhi walā tahzan 'alayhim walā taku fī dayqim mimmā yamkurūn

Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya MwenyeziMungu tu. Wala usiwahuzunikie; wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya. 127

Maelezo ya chini

127 Na ewe Nabii! Subiri! Kwani hivyo ndio yatakusahilikia mengi katika mashaka ya maisha, na yataondoka matatizo yake. Wala usisikitike kwa kuwa watu wako hawaitikii Wito wako, na hawakuamini. Wala usione dhiki kifuani mwako kwa hila zao na vitimbi vyao vya kuukaba roho Wito wako. Kwani vitendo vyao havitakudhuru kitu. Na wewe umekwisha tekeleza waajibu wako, na umemcha Mola wako Mlezi.