Surat An-Nahl, aya 126

16:126

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ ١٢٦

Wa in 'āqabtum fa'āqibū bimithli mā 'ūqibtum bihī wala'in sabartum lahuwa khayrul lis-sābirīn

Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri. 126

Maelezo ya chini

126 Enyi Waislamu! Mkitaka kuwaadhibu wale wanao kufanyieni uadui wakakuvamieni, basi waadhibuni kwa kadiri walivyo kutendeeni, wala msizidishe kuliko hivyo. Na kuweni na yakini kwamba mkistahamili, msijilipizie kisasi, itakuwa ni kheri zaidi kwenu hapa duniani na Akhera. Basi toeni adhabu kwa ajili ya Haki, wala msiadhibu kwa ajili ya nafsi zenu.