إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ ١٢٨
Innallāha ma'al-ladhīnat-taqaw wwalladhīna hum muhsinūn
Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema. . 128
Maelezo ya chini
128 Kwani hakika Mola wako Mlezi yu pamoja na wale wanao jikinga na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyaepuka anayo yakataza, na wakazifanya a'mali zao ziwe nzuri kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kwa kukubali kumt'ii. Yeye atawanusuru duniani, na Akhera atawalipa bora ya malipo.