Surat An-Nahl, aya 12

16:12

وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ ١٢

Wasakkhara lakumul-layla wan-nahāra wash-shamsa wal-qamara wan-nujūmu musakkharātu bi amrihī inna fī dhālika la'āyātil liqawmin ya'qilūn

Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi,na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili. 12

Maelezo ya chini

12 Na Mwenyezi Mungu ameufanya usiku ukutumikieni kwa kuufanya uwe ndio wakati wenu wa kupumzika na mchana ni muwafaka kuhangaika kwenu na kwenda kwa kazi zenu, na jua kukuleteeni joto na mwangaza, na mwezi mpate kujua idadi ya miaka na hisabu, na nyota zinazo kutumikieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu ili mpate kujua njia katika kiza. Hakika katika hayo zipo alama na dalili kwa watu ambao wananufaika kwa akili aliyo wapa Mwenyezi Mungu.