وَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۘ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ كُلُّ شَيۡءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجۡهَهُۥۚ لَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٨٨
Walā tad'u ma'allāhi ilāhan ākhara lā ilāha illā huwa kullu shay'in hālikun illā wajhahū lahul-hukmu wa ilayhi turja'ūn
Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwenginewe. Hapana mungu ila Yeye. Kila kitu kitaangamia isipo kuwa Yeye. Hukumu iko kwake, na kwake mtarejezwa. 88
Maelezo ya chini
88 Wala usimwabudu mungu yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwani hapana kabisa mungu wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye. Kila kitu isipo kuwa Mwenyezi Mungu kitaangamia na kwisha. Wa kudumu milele ni Yeye Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye mwenye hukumu ya kutekeleza duniani na Akhera. Na kwake Yeye ndiyo yako marejeo ya viumbe vyote, hapana hivi wala hivi.