وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بَعۡدَ إِذۡ أُنزِلَتۡ إِلَيۡكَۖ وَٱدۡعُ إِلَىٰ رَبِّكَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ٨٧
Walā yasuddunnaka 'an āyātillāhi ba'da idh unzilat ilayka wad'u ilā rabbika walā takūnanna minal-mushrikīn
Wala wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na lingania kwa Mola wako Mlezi, wala usiwe miongoni mwa washirikina. 87
Maelezo ya chini
87 Wala makafiri wasikuachishe kuzifikisha Aya za Mwenyezi Mungu na kuzitenda, baada ya kwisha teremka wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ukawa ndio Ujumbe wako. Na shikilia Wito kuwaitia watu kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu. Wala usiwe wewe wala wanao kufuata katika wasaidizi wa washirikina kwa kuwasaidia kwa wayatakayo.