Surat Al-Qasas, aya 80

28:80

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ وَيۡلَكُمۡ ثَوَابُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّمَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗاۚ وَلَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلصَّٰبِرُونَ ٨٠

Waqālal-ladhīna ūtul-'ilma waylakum thawābullāhi khayrul liman āmana wa'amila sālihan walā yulaqqāhā illas-sābirūn

Na wakasema wale walio pewa ilimu: Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye subira. 80

Maelezo ya chini

80 Ama wale ambao Mwenyezi Mungu amewaruzuku ilimu yenye manufaa hawakusalitika na hayo. Wakawaelekea walio danganyika kwa kuwanasihi wakiwaambia: Msiyatamani haya, wala msiiache Dini. Kwani yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya thawabu na neema ni safi zaidi kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Na hiyo ni nasiha ya kweli ambayo hawaikubali ila wenye kuzipiga jihadi nafsi zao, na wakasubiri katika ut'iifu.