وَرَبُّكَ يَعۡلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمۡ وَمَا يُعۡلِنُونَ ٦٩
Warabbuka ya'lamu mā tukinnu sudūruhum wamā yu'linūn
Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. 69
Maelezo ya chini
69 Ewe Mtume! Mola wako Mlezi anajua baraabara yaliomo katika vifua vya washirikina ya uadui wao juu yako, na wanayo tangaza kwa ndimi zao ya kukushutumu na kukupinga kwa ulivyo teuliwa kupewa Utume.