وَهُوَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأُولَىٰ وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٧٠
Wahuwallāhu lā ilāha illā huwa lahul-hamdu fil-ūlā wal-ākhirati walahul-hukmu wa ilayhi turja'ūn
Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa. 70
Maelezo ya chini
70 Na Mola wako Mlezi, ewe Mtume, ndiye Mwenyezi Mungu wa Haki, ndiye pekee Mwenye Ungu, Mwenye kustahiki peke yake kuhimidiwa na waja wake katika dunia kwa neema zake na uwongofu wake, na katika Akhera kwa uadilifu wake na kulipa kwake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye hukumu, na kuamua baina ya waja wake. Na kwake Yeye ndiyo marejeo ya kwendea.