Surat Al-Qasas, aya 68

28:68

وَرَبُّكَ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخۡتَارُۗ مَا كَانَ لَهُمُ ٱلۡخِيَرَةُۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ٦٨

Warabbuka yakhluqu mā yashā'u wayakhtāru mā kāna lahumul-khiyaratu subhānallāhi wata'ālā 'ammā yushrikūn

Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye. 68

Maelezo ya chini

68 Na Mola wako Mlezi anaumba atakalo kwa uwezo wake. Na anamkhitari amtakaye kwa hikima yake kumpa Ujumbe na ut'iifu kwa kujua kwake mwenyewe kufaa kwao. Wala hawawezi viumbe, na wala si haki, kumchagulia Mwenyezi Mungu walitakalo katika dini potovu, na miungu ya uwongo. Mtukufu ametakasika shani yake na washirika.