فَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلۡمُفۡلِحِينَ ٦٧
Fa ammā man tāba wa āmana wa'amila sālihan fa'asā an yakūna minal-muflihīn
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufanikiwa. 67
Maelezo ya chini
67 Hii ndiyo hali ya washirikina. Ama mwenye kutubu kutokana na shirki yake, na akaamini Imani ya kweli, na akatenda mema, basi huyo hutaraji kuwa kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa walio fuzu kuipata radhi ya Mwenyezi Mungu, na neema ya kudumu yenye kuendelea milele.