Surat Al-Qasas, aya 50

28:50

فَإِن لَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكَ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيۡرِ هُدٗى مِّنَ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ٥٠

Fa il lam yastajībū laka fa'lam annamā yattabi'ūna ahwā'ahum waman adallu mimmanit-taba'a hawāhu bighayri hudam minallāhi innallāha lā yahdil-qawmaz-zālimīn

Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. 50

Maelezo ya chini

50 Na ikiwa hawaitikii wito wako kwa kuleta kitabu kiongofu zaidi, basi jua kuwa wamebanwa na hawakubakiliwa na hoja yoyote, na kwamba kwa hayo wanafuata pumbao zao tu. Na hapana aliye zidi kwa upotovu kuliko yule anaye fuata pumbao lake katika dini, bila ya uwongofu kutokana na Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hamwafiki mwenye kuidhulumu nafsi yake kwa kufuata upotovu bila ya kuitafuta Haki.