Surat Al-Qasas, aya 49

28:49

قُلۡ فَأۡتُواْ بِكِتَٰبٖ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ هُوَ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمَآ أَتَّبِعۡهُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٤٩

Qul fa tū bikitābim min 'indillāhi huwa ahdā minhumā attabi'hu in kuntum sādiqīn

Sema: Basi leteni Kitabu kinacho toka kwa Mwenyezi Mungu chenye kuongoka zaidi kuliko hivi viwili tukifuate, kama nyinyi mnasema kweli. 49

Maelezo ya chini

49 Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hamuiamini Taurati na Qur'ani basi leteni kitabu kingine kinacho toka kwa Mwenyezi Mungu kilicho na uwongofu bora kuliko hivyo, au kama hivyo, nami nikifuate pamoja nanyi, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika hayo madai yenu kwamba tuliyo kuja nayo ni uchawi.