وَأَصۡبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَٰرِغًاۖ إِن كَادَتۡ لَتُبۡدِي بِهِۦ لَوۡلَآ أَن رَّبَطۡنَا عَلَىٰ قَلۡبِهَا لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٠
Wa asbaha fu'ādu ummi mūsā fārighan in kādat latubdī bihī lawlā ar rabatnā 'alā qalbihā litakūna minal-mu'minīn
Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini. 10
Maelezo ya chini
10 Na mama yake Musa akawa hajitambui kwa dhiki iliyo muingia kwa kuwa mwanawe kaangukia mikononi mwa Firauni. Akawa anakurubia kujitambulisha kwamba yeye ndiye mama yake. Lau ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakuutia imara moyo wake kwa kusubiri, basi angeli tangaza kuwa huyo ni mwanawe, jinsi alivyo kuwa akimhurumia, na pia ili awe miongoni mwa Waumini wenye kutulia.