Surat Al-Qasas, aya 9

28:9

وَقَالَتِ ٱمۡرَأَتُ فِرۡعَوۡنَ قُرَّتُ عَيۡنٖ لِّي وَلَكَۖ لَا تَقۡتُلُوهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٩

Waqālatimra'atu fir'awna qurratu 'aynil lī walaka lā taqtulūhu 'asā an yanfa'anā aw nattakhidhahū waladan wahum lā yash'urūn

Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua. 9

Maelezo ya chini

9 Mke wa Firauni alipo mwona mtoto alimwambia mumewe: Mtoto huyu atatuletea furaha mimi na wewe. Tumweke, tusimuuwe, kwa kutaraji kuwa atakuja tufaa kuendesha mambo yetu. Au tumfanye mwenetu wa kumlea. Na wao kumbe hawatambui aliyo mkadiria Mwenyezi Mungu.