ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ ٣
Dhālika bi annahum āmanū thumma kafarū fatubi'a 'alā qulūbihim fahum lā yafqahūn
Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote. 3
Maelezo ya chini
3 Hayo waliyo yafanya ndiyo mazoea ya kudhihirisha yasiyo ya kweli, na kuapa yamini za uwongo, kwa sababu hao wameamini kwa ndimi zao, kisha wakakufuru katika nyoyo zao, basi nyoyo zao zimepigwa muhuri kwa ukafiri huu. Hao hawafahamu yepi ya kuwaokoa na adhabu za Mwenyezi Mungu.