لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ٣
Lan tanfa'akum arhāmukum walā awlādukum yawmal-qiyāmati yafsilu baynakum wallāhu bimā ta'malūna basīr
Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. 3
Maelezo ya chini
3 Hawatakufaeni kitu jamaa zenu wala watoto wenu mlio wafanya kuwa ni marafiki, na hali wao ni adui wa Mwenyezi Mungu na adui zenu. Katika Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atakutengeni mbali mbali. Atawatia maadui zake Motoni na marafiki zake Peponi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote myatendayo.