Surat Al-Mumtahanah, aya 2

60:2

إِن يَثۡقَفُوكُمۡ يَكُونُواْ لَكُمۡ أَعۡدَآءٗ وَيَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ وَأَلۡسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ ٢

In yathqafūkum yakūnū lakum a'dā'an wayabsutū ilaykum aydiyahum wa alsinatahum bis-sū'i wawaddū law takfurūn

Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri. 2

Maelezo ya chini

2 Wakikutana nanyi na wakakuwezeni, uadui wao kwenu unadhihiri, na wanakunyoosheeni mikono yao na ndimi zao kukudhuruni. Na wanatamani muwe makafiri kama wao.