Surat Al-Mujadilah, aya 10

58:10

إِنَّمَا ٱلنَّجۡوَىٰ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ لِيَحۡزُنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَيۡسَ بِضَآرِّهِمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ١٠

Innaman-najwā minash-shaytāni liyahzunal-ladhīna āmanū walaysa bidārrihim shay'an illā bi idhnillāhi wa'alallāhi falyatawakkalil-mu'minūn

Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walio amini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini. 10

Maelezo ya chini

10 Hakika kusema siri kwa kuchochea shaka shaka ni katika kuzainishwa na Shetani, ili apate kuingiza huzuni katika nyoyo za Waumini. Wala hayo hayawezi kuwaletea madhara yoyote wao ila kwa kupenda Mwenyezi Mungu. Basi Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu peke yake.