وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَٱحۡذَرُواْۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ٩٢
Wa atī'ullāha wa atī'ur-rasūla wahdharū fa in tawallaytum fa'lamū annamā 'alā rasūlinal-balāghul-mubīn
Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi. 92
Maelezo ya chini
92 Na fuateni amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake kwa yale anayo kuleteeni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Na yaepukeni mbali yatakayo kuleteeni adhabu mnapo kwenda kinyume. Mkitofuata anayo kuamrisheni Mwenyezi Mungu kuweni na yakini kuwa Yeye atakupeni adabu. Wala nyinyi hamna udhuru wowote baada ya kuwa Mtume amekwisha wabainishieni adabu ya kupewa wakhalifu. Na hakika haimpasi Mtume wetu ila kukujuvyeni hukumu zetu tu, na kukubainishieni kwa ukamilifu wa uwazi.