Surat Al-Ma'idah, aya 49

5:49

وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ ٤٩

Wa anihkum baynahum bimā anzalallāhu walā tattabi' ahwā'ahum wahdharhum an yaftinūka 'am ba'di mā anzalallāhu ilayka fa in tawallaw fa'lam annamā yurīdullāhu an yusībahum biba'di dhunūbihim wa inna kathīram minan-nāsi lafāsiqūn

Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu. 49

Maelezo ya chini

49 Na wewe ewe Mtume! Tumekuamrisha uhukumu baina ya watu kwa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matakwa yao katika kuhukumu. Na wahadharishe wasije kukugeuza ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Pindi wakiipuuza hukumu ya Mwenyezi Mungu na wakataka nyengineyo, basi jua kuwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapatiliza kwa kuwafisidia mambo yao, kwa vile zilivyo kwisha fisidika nafsi zao kwa sababu ya madhambi yao waliyo yatenda kwa kukhalifu hukumu zake na Sharia yake. Kisha atawalipa vitendo vyao vyote huko Akhera. Na hakika watu wengi ni wenye kuziasi hukumu za Sharia. Maneno haya yanatukuza Sharia ya Kiislamu katika kuwahukumu watu. Kwanza inatukuka kwa kuwa ni hukumu ya uadilifu na haifuati mipango ya watu ijapo kuwa ni mipotovu, bali inahukumu juu ya hiyo mipango ya watu kwa kheri na shari. Pili Kanuni huwa katika dola ni moja tu kwa watu wote na mat'abaka yote.