Surat Al-Ma'idah, aya 39

5:39

فَمَن تَابَ مِنۢ بَعۡدِ ظُلۡمِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَتُوبُ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ٣٩

Faman tāba mim ba'di zulmihī wa aslaha fa innallāha yatūbu 'alayhi innallāha ghafūrur rahīm

Lakini mwenye kutubia baada ya dhulma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu atapokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 39

Maelezo ya chini

39 Lakini mwenye kutubu baada ya kutenda kosa lake hilo, na akatengeneza vitendo vyake, na akanyoosha mwendo wake, basi Mwenyezi Mungu hakika humkubalia toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi mno wa kusamehe na kurehemu.