Surat Al-Ma'idah, aya 35

5:35

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱبۡتَغُوٓاْ إِلَيۡهِ ٱلۡوَسِيلَةَ وَجَٰهِدُواْ فِي سَبِيلِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ٣٥

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanut-taqullāha wabtaghū ilayhil-wasīlata wajāhidū fī sabīlihī la'allakum tuflihūn

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka. 35

Maelezo ya chini

35 Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kwa kujitenga na anayo yakataza, na kut'ii amri zake. Na takeni kuyafanya yatakayo kukurubisheni kupata thawabu zake, nayo ni kutenda mambo ya ut'iifu na mambo ya kheri. Na wanieni kwa jihadi katika Njia yake kwa kuitukuza Dini yake na kuwapiga vita maadui zake. Huenda kwa hivyo mkafuzu mkapata karama zake na thawabu zake.