Surat Al-Ma'idah, aya 34

5:34

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِن قَبۡلِ أَن تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهِمۡۖ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٣٤

Illal-ladhīna tābū min qabli an taqdirū 'alayhim fa'lamū annallāha ghafūrur rahīm

Isipo kuwa wale walio tubu kabla hamjawatia nguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 34

Maelezo ya chini

34 Ila wale walio tubu, miongoni mwa hawa wanao piga vita nidhamu na wakavamia watu majiani, kabla hamjawatia mkononi mkawakamata. Basi adhabu ya Mwenyezi Mungu itaondoka, itabaki juu yao haki za waja wa Mwenyezi Mungu wazirejeshe. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na rehema. Katika hukumu hii inabainishwa kuwa Sharia inaangalia ukhalifu unao athiri jamii, na kwa hivyo adhabu yake ni kali kwa kuwafikiana na kitisho chake kwa wapendao amani. Mazingatio hapa si kwa mujibu wa kile kitendo cha ukhalifu, bali kwa mujibu wa kiasi ya kitisho na fazaa inayo letwa na hicho kitendo.