Surat Al-Ma'idah, aya 14

5:14

وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰٓ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَهُمۡ فَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَأَغۡرَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَاوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَسَوۡفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ ١٤

Waminal-ladhīna qālū innā nasārā akhadhnā mīthāqahum fanasū hazzam mimmā dhukkirū bihī fa aghraynā baynahumul-'adāwata wal-baghdā'a ilā yawmil-qiyāmati wasawfa yunabbi'uhumullāhu bimā kānū yasna'ūn

Na kutoka kwa wale walio sema: Sisi ni Manasara, tulichukua ahadi yao, lakini wakasahau sehemu ya waliyo kumbushwa. Kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya. 14

Maelezo ya chini

14 Hali kadhaalika Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa Wakristo, ambao wamesema: Sisi ni Manasara, kwa kuwa wataiamini Injili, na watamuamini Mwenyezi Mungu Mmoja. Nao wakaacha mengi walio amrishwa katika Injili. Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa hayo, kwa kutia uadui na khasama baina ya wao kwa wao, wakawa makundi mbali mbali yenye uadui mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya, na atawalipa kwayo.