يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ كَثِيرٗا مِّمَّا كُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِيرٖۚ قَدۡ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٞ وَكِتَٰبٞ مُّبِينٞ ١٥
Yā'ahlal-kitābi qad jā'akum rasūlunā yubayyinu lakum kathīram mimmā kuntum tukhfūna minal-kitābi waya'fū 'an kathīrin qad jā'akum minallāhi nūrun wakitābum mubīn
Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. 15
Maelezo ya chini
15 Enyi Watu wa Kitabu! Amekujilieni Mtume wetu, Muhammad, akiita watu wafuate Haki. Anakufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Taurati na Injili. Na anayaacha mengi katika mliyo yaficha ambayo hayana haja kuyadhihirisha. Amekuleteeni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Sharia kaamili, ambayo Sharia hiyo peke yake ni nuru, na inabainishwa na Kitabu kilicho wazi.