۞ وَلَقَدۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَبَعَثۡنَا مِنۡهُمُ ٱثۡنَيۡ عَشَرَ نَقِيبٗاۖ وَقَالَ ٱللَّهُ إِنِّي مَعَكُمۡۖ لَئِنۡ أَقَمۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَيۡتُمُ ٱلزَّكَوٰةَ وَءَامَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرۡتُمُوهُمۡ وَأَقۡرَضۡتُمُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّكُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ فَمَن كَفَرَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ ١٢
Walaqad akhadhallāhu mīthāqa banī isrā'īla waba'athnā minhumuthnay 'ashara naqīban waqālallāhu innī ma'akum la in aqamtumus-salawāta wa ātaytumuz-zakawāta wa āmantum birusulī wa'azzartumūhum wa aqradtumullāha qardan hasanal la ukaffiranna 'ankum sayyi'ātikum wala'udkhilannakum jannātin tajrī min tahtihal-anhāru faman kafara ba'da dhālika minkum faqad dalla sawā'as-sabīl
Na Mwenyezi Mungu alifanya agano na Wana wa Israili. Na tukawateulia kutokana nao wakuu kumi na mbili. Na Mwenyezi Mungu akasema: Kwa yakini Mimi ni pamoja nanyi. Mkisali, na mkatoa Zaka, na mkawaamini Mitume wangu, na mkawasaidia, na mkamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, hapana shaka nitakufutieni maovu yenu na nitakuingizeni katika mabustani yapitayo mito kati yake. Lakini atakaye kufuru miongoni mwenu baada ya hayo bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa. 12
Maelezo ya chini
12 Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kutokana na Wana wa Israili kuwa watamsikia na watamt'ii. Akawateulia marais thinaashara (kumi na mbili) kutokana miongoni mwao ili itimie hiyo ahadi. Na Yeye Mwenyezi Mungu akawaahidi ahadi ya nguvu kuwa atakuwa pamoja nao, atawasaidia na atawanusuru ikiwa watashika Swala kama ipasavyo, na watatoa Zaka walizo faridhiwa, na watawasadiki Mitume wake wote, na watawanusuru, na watatoa mali kwa ajili ya mambo ya kheri. Na kwamba pindi wakifanya hayo basi Mwenyezi Mungu atawafutia dhambi zao, na atawatia katika Bustani zake zipitazo mito kati yake. Na mwenye kukufuru, na akavunja ahadi baada ya hayo, basi huyo amepotoka na hakufuata njia iliyo kaa sawa iliyo nyooka.