Surat Al-Ma'idah, aya 11

5:11

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ هَمَّ قَوۡمٌ أَن يَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ فَكَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ١١

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanudhkurū ni'matallāhi 'alaykum idh hamma qawmun an yabsutū ilaykum aydiyahum fakaffa aydiyahum 'ankum wattaqullāha wa'alallāhi falyatawakkalil-mu'minūn

Enyi mlio amini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, walipo taka watu kukunyooshieni mikono, naye akaizuilia mikono yao kukufikieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. 11

Maelezo ya chini

11 Enyi Waumini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu katika wakati wa shida, pale baadhi ya Washirikina walipo kusudia kukuuweni nyinyi na Mtume wenu, Mwenyezi Mungu akazuia balaa yao isikufikieni, na akakuokoeni. Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na mumtegemee Yeye peke yake, katika mambo yenu. Kwani Yeye anakutosheni. Inavyo muelekea Muumini ni kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake daima milele.