يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَوۡفُواْ بِٱلۡعُقُودِۚ أُحِلَّتۡ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلۡأَنۡعَٰمِ إِلَّا مَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ غَيۡرَ مُحِلِّي ٱلصَّيۡدِ وَأَنتُمۡ حُرُمٌۗ إِنَّ ٱللَّهَ يَحۡكُمُ مَا يُرِيدُ ١
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū awfū bil-'uqūdi uhillat lakum bahīmatul-an'āmi illā mā yutlā 'alaykum ghayra muhillis-saydi wa antum hurumun innallāha yahkumu mā yurīd
Enyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo. 1
Maelezo ya chini
1 Enyi Waumini! Jilazimisheni kutimiza ahadi zote baina yenu na Mwenyezi Mungu, na ahadi za kisharia zilio baina yenu na watu wengineo. Na Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kula nyama howa, yaani nyama wa kufuga, kama ngamia, ng'ombe, kondoo, mbuzi n.k. ila wale mlio tajiwa kuwa ni haramu. Wala haikujuzieni kuwinda barani pale mnapo kuwa mmeharimia Hija, au mpo katika eneo la ardhi takatifu. Hakika Mwenyezi Mungu huhukumu apendavyo kwa hikima yake. Yeye ndiye Muumbaji, na ndiye Mwenye kujua jema na baya la viumbe vyake. Na haya ni miongoni mwa ahadi za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu.