Surat Al-Kahf, aya 59

18:59

وَتِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰٓ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡ لَمَّا ظَلَمُواْ وَجَعَلۡنَا لِمَهۡلِكِهِم مَّوۡعِدٗا ٥٩

Watilkal-qurā ahlaknāhum lammā zalamū waja'alnā limahlikihim maw'idā

Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipo dhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao. 59

Maelezo ya chini

59 Na hii basi ndio miji ya kale tuliyo iteketeza pale watu wao walipo dhulumu kwa kuwakanusha Mitume wao. Na Sisi tukawawekea miadi ya kuwaangamiza isiyo na khitilafu. Hali kadhaalika itakuwa ya hao katika kaumu yako wanao kanusha, ikiwa hawaamini.