وَكَانَ لَهُۥ ثَمَرٞ فَقَالَ لِصَٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَنَا۠ أَكۡثَرُ مِنكَ مَالٗا وَأَعَزُّ نَفَرٗا ٣٤
Wakāna lahū thamarun faqāla lisāhibihī wahuwa yuhāwiruhū ana aktharu minka mālan wa a'azzu nafarā
Naye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu! 34
Maelezo ya chini
34 Na huyo mwenye vitalu alikuwa na mali mengine yenye kutoa mazao yake pia. Basi ikamuingia ghururi kwa neema ile. Katika ile ghururi yake akamwambia mwenzie yule Muumini nao walikuwa wakijadiliana: Mimi nina mali mengi kuliko wewe, na ninakushinda kwa nguvu za jamaa zangu na wasaidizi.