نَّحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ نَبَأَهُم بِٱلۡحَقِّۚ إِنَّهُمۡ فِتۡيَةٌ ءَامَنُواْ بِرَبِّهِمۡ وَزِدۡنَٰهُمۡ هُدٗى ١٣
Nnahnu naqussu 'alayka naba'ahum bil-haqqi innahum fityatun āmanū birabbihim wazidnāhum hudā
Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu. 13
Maelezo ya chini
13 Ewe Mtume! Sisi tunakusimulia khabari zao kweli kweli: Hakika hao walikuwa vijana katika zama zilizo pita ambao walikuwa wameshika Dini ya Haki. Walimuamini Mola wao Mlezi kuwa ni Mmoja tu, na ilihali wamezungukwa na washirikina.