Surat Al-Jumu'ah, aya 11

62:11

وَإِذَا رَأَوۡاْ تِجَٰرَةً أَوۡ لَهۡوًا ٱنفَضُّوٓاْ إِلَيۡهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمٗاۚ قُلۡ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ مِّنَ ٱللَّهۡوِ وَمِنَ ٱلتِّجَٰرَةِۚ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ ١١

Wa idhā ra'aw tijāratan aw lahwaninfaddū ilayhā watarakūka qā'iman qul mā 'indallāhi khayrum minal-lahwi waminat-tijārati wallāhu khayrur-rāziqīn

Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki. 11

Maelezo ya chini

11 Na wakiona bidhaa za biashara, au pumbao lolote hutawanyika kuendea hayo, na wakakuacha wewe umesimama unakhutubu! Waambie: Fadhila na thawabu zilioko kwa Mwenyezi Mungu zina nafuu zaidi kwenu kuliko pumbao na kuliko biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanao toa riziki. Basi itafuteni riziki yake kwa kumt'ii Yeye.