۞ ٱللَّهُ ٱلَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡبَحۡرَ لِتَجۡرِيَ ٱلۡفُلۡكُ فِيهِ بِأَمۡرِهِۦ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ١٢
Allāhul-ladhī sakkhara lakumul-bahra litajriyal-fulku fīhi bi amrihī walitabtaghū min fadlihī wala'allakum tashkurūn
Mwenyezi Mungu ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite marikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru. 12
Maelezo ya chini
12 Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ikutumikieni bahari ili marikebu zipate kwenda juu yake kwa idhini yake, na uwezo wake, zikikubebeni nyinyi na bidhaa zenu, na ili mtafute kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu mali ya baharini kwa kupata manufaa ya ujuzi, na biashara, na jihadi, na zawadi, na uvuvi, na kutoa vyombo, na ili mpate kushukuru neema zake kwa kumsafia Dini Mwenyezi Mungu.