Surat Al-Jathiyah, aya 13

45:13

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مِّنۡهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ ١٣

Wasakkhara lakum mā fis-samāwāti wamā fil-ardi jamī'am minhu inna fī dhālika la'āyātil liqawmin yatafakkarūn

Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. 13

Maelezo ya chini

13 Na akakudhalilishieni vyote viliomo mbinguni, nyota zenye kung'ara na sayari, na vyote viliomo kwenye ardhi, makulima, mifugo, maji, moto, hewa, na jangwa, vyote hivyo vinatokana na Yeye Mtukufu, ili akuenezeeni manufaa ya uhai. Hakika katika hizo neema zilizo tajwa zipo Ishara zenye kuonyesha kudra yake kwa watu wenye kuzingatia Ishara.