وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا ٨٩
Walaqad sarrafnā lin-nāsi fī hādhal-qur'āni min kulli mathalin fa abā aktharun-nāsi illā kufūrā
Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur'ani kwa kila mfano. Lakini watu wengi wanakataa isipo kuwa kukanusha tu. 89
Maelezo ya chini
89 Na katika Qur'ani hii tumewaeleza watu kwa namna mbali mbali kila maana kama ni mifano katika maajabu yake. Lakini watu wengi walikataa ila kupinga na kuchukia.