وَقَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفۡجُرَ لَنَا مِنَ ٱلۡأَرۡضِ يَنۢبُوعًا ٩٠
Waqālū lan nu'mina laka hattā tafjura lanā minal-ardi yambū'ā
Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. 90
Maelezo ya chini
90 Ilipo dhihiri kushindwa kwao na Qur'ani, na wakabanwa kwa hoja, wakataka waletewe ishara nyingine na miujiza mingine. Hicho ni kitendo cha mwenye kushindwa hoja, aliye emewa na kutahayari. Ndio wakasema: Hatutokuamini mpaka ututimbulie katika ardhi ya Makka chemchem ambayo maji yake hayakatiki.