Surat Al-Isra, aya 70

17:70

۞ وَلَقَدۡ كَرَّمۡنَا بَنِيٓ ءَادَمَ وَحَمَلۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَفَضَّلۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ كَثِيرٖ مِّمَّنۡ خَلَقۡنَا تَفۡضِيلٗا ٧٠

Walaqad karramnā banī ādama wahamalnāhum fil-barri wal-bahri warazaqnāhum minat-tayyibāti wafaddalnāhum 'alā kathīrim mimman khalaqnā tafdīlā

Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba. 70

Maelezo ya chini

70 Na hakika Sisi tumewatukuza wana wa Adam kwa kuwapa umbo zuri lilio nyooka, na matamshi, na uwezo wa kukhiari mambo. Na tukawapa hishima na utukufu pindi wakit'ii. Na tukawapakia nchi kavu juu ya wanyama, na baharini katika marikebu, na tukawaruzuku vitu vitamu, na tukawafadhilisha fadhila kubwa kuliko viumbe vingi kwa kuwapa akili na kuweza kufikiri.