أَمۡ أَمِنتُمۡ أَن يُعِيدَكُمۡ فِيهِ تَارَةً أُخۡرَىٰ فَيُرۡسِلَ عَلَيۡكُمۡ قَاصِفٗا مِّنَ ٱلرِّيحِ فَيُغۡرِقَكُم بِمَا كَفَرۡتُمۡ ثُمَّ لَا تَجِدُواْ لَكُمۡ عَلَيۡنَا بِهِۦ تَبِيعٗا ٦٩
Am amintum an yu'īdakum fīhi tāratan ukhrā fayursila 'alaykum qāsifam minar-rīhi fayughriqakum bimā kafartum thumma lā tajidū lakum 'alaynā bihī tabī'ā
Au mmeaminisha ya kuwa hatakurudisheni humo mara nyengine na kukupelekeeni kimbunga cha upepo akakuzamisheni kwa mlivyo kufuru, na kisha msipate wa kukunusuruni nasi. 69
Maelezo ya chini
69 Au nyinyi mmeaminisha kuwa Mola wenu Mlezi hatakurejesheni tena baharini, na akuleteeni tufani la upepo livunjilie mbali hicho chombo chenu? Akakuzamisheni kwa sababu ya kuto thamini neema yake pale alipo kuokoeni mara ya kwanza? Tena hapo hamtapata wa kukuteteeni kwetu kwa tuliyo kufanyieni ili mpate kusalimika.